19 Machi 2011 - 20:30

Baada ya kupita siku kadhaa za kunyamazia kimya hatua ya Iran ya kuteka ndege ya kijasusi ya Marekani ndani ya ardhi ya Iran, Rais Barack Obama wa Marekani ameibuka na kusema kuwa Washington imeiomba Tehran iirejeshee ndege hiyo.

Tumewaomba waturejeshee. Tunasubiri kuona Wairani watajibu nini," amesema Obama katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki jana Jumatatu.Viongozi wa Marekani walioonekana kuchanganyikiwa baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuiteka ndege ya kisasa kabisa ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170 isiyoonekana kwa rada, wakati ilipokuwa inafanya ujasusi mashariki mwa Iran, sasa wameamua kutokaa tena kimya hasa baada ya Iran kuonyesha video inayothibitisha kuwa ndege hiyo imetekwa na Iran baada ya kutiwa dosari ndogo tu.Tayari Iran imesema kuwa kamwe haiwezi kurejesha ndege hiyo na tayari imeshachukua hatua mbalimbali za kuishitaki Marekani kwa kuingia bila ruhusa kwenye anga ya Iran na kwa kufanya ujasusi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.